Watu
wengi wanakufa masikini na wanashindwa kufikia mafanikio yao bila wao
kujua tatizo ni nini,imekuwa kama ugonjwa watu wengi kuendelea
kulalamikia serikali au wazazi wao kuwa wao hawafanikiwi wao ndio
sababu,na wengine wamekuwa wakikata tamaa kabisa ya mafanikio yao bila
wao kujua nini kinachokwamisha maisha yao kuwa bora.Leo tutajifunza
pamoja vizuwizi vya mafanikio yako ambapo kama utavifanyia kazi basi
utaanza kushuhudia mafanikio yako,ni muujiza mkubwa sana utatokea kwako
hakuna aliezaliwa kuwa masikini rafiki.soma kwa makini.
1.UOGA(Fear)
Hichi ni kikwazo kikubwa sana kwa watu wengi ktk mafanikio yao,watu
wengi wamekuwa masikin na wengine kufa masikin kwasababu ya uoga,uoga wa
kukataliwa na uoga wa kushindwa,kama unataka kufanikiwa ktk kila kitu
kwenye maisha yako usiogope kuomba au kusema chochote mbele ya watu eti
kwa kuogopa kukataliwa rafiki usiusemee moyo wa mwenzio usiogope,lkn pia
usiogope kushindwa yani mtu anataka kufanyabiashara lkn kitu cha
kwanza anawaza ni kushindwa anaamini kuwa yeye hawezi na akianzisha
atafeli.Rafiki acha uoga kwani huo ndio umasikin wako ushinde uoga
ushinde maishani.USIOGOPE..
2. KUKOSA MSUKUMO (Lack of agressivenes)
Watu wengi wanashindwa kufanikiwa ktk maisha yao kwa sababu ya kukosa
msukumo binafsi,ngoja nikwambie rafiki hakuna mtu yeyote ambae atakaa
chini na kupanga maisha yako au kuna mtu ataacha shughuli zake kwaajili
ya kupigania maisha yako,wewe ndio unaejua ugumu na uchungu wa maisha
yako amka sasa kuwa na msukumo kutoka moyoni mwako wa kushinda maishani
usisubiri fulani ndo akwambie nenda kazi,fanyabiashara wewe mwenyewe kaa
chini jitume utafanikiwa.
3.UJASIRI NA KUJIAMIN (Courage and confidance)
Hpa ndipo balaa watanzania wengi hawajiamini rafiki hebu jiamini kuwa
wewe unaweza ndani yako kuna mtu mkubwa saana,hebu acha kusikiliza watu
wengine wanasema nini kuhusu wewe usikilize moyo wako unasema nini
kuhusu wewe,usikubali kushindwa thubutu kwa kila jambo unaloambiwa
lenye mafanikio na usiamini kuwa wewe huwezi unaweza rafiki.
4.KUKOSA LENGO MAALUMU (Lack of purpose driven goals)
Rafiki malengo yako nini? Lengo ni ndoto zenye mipaka,kuna malengo ya
muda mfupi,muda mrefu na muda wa kati.wewe malengo yako ni yapi? rafiki
hautakuja kufanikiwa ktk maisha yako kama huna malengo ya maisha yako
kama huna malengo panga leo yaandike malengo yako.mtu asiye na malengo
ni sawa na mtu ambae anaenda stendi kupanda gari lkn hajui anaenda wapi
sasa atapanda gari gani na atashukia wapi huyu hata fika bali
atazunguuka a ari hadi usiku gari linapokwenda kupaki basi litamshusha
popote.JUA MALENGO YAKO RAFIKI UTAFANIKIWA.
5.KUTOKUJITOA (Lak of comittment)
Kujitoa limekuwa tatizo kwa watanzania wengi, ewe mtanzania jitoe
kwaajili ya maisha yako acha uvivu wa kufikiria Mungu ashughuliki na
wavivu jitoe pambana kwaajili ya maisha yako utafanikiwa.
6.KULINDA MUDA (Timemanagement)
Hahahahaaaa watu wengi wanaposikia mua ni mali huwa hawaamini leo
nataka ujue kuwa muda wako ndio umasikini wako na ndio utajiri
wako.unatumiaje muda wako ambao unatoka kazini? unatumiaje muda wako
ambao unatocha chuo? wewe mama wa nyumbani unatumiaje muda wako ambao
unakuwa hauna kazi nyumbani? hapa ndipo kasheshe na umasikini wa watu
ulipo.iko kila sekunde na saa inayopita lazima uhakikishe unafanya kitu
ambacho chenye manufaa kwenye maisha yako,mfano ukitumia masaa mawili
unajifunza kitu chenye mafanikio kwenye maisha yako basi unayavuta
mafanikio yako masaa mawili kama mafanikio yako yalikuwa uyafikie kwa
siku mbili na masaa mawili basi utakuwa umebakisha siku mbili.kama
unatumia muda wako kuangalia TV,kupiga umbea kupiga story zisizokuwa na
maana ukifanya hivyo masaa mawili kwa siku ndani ya mwaka utakuwa
umepoteza zaidi ya miezi 4,basi hiyo miezi minne ndio umesogeza mbele
mafanikio yako.kwaiyo kama ungetakiwa ufanikiwe kwa miaka miwili basi
utafanikiwa kwa miaka miwili na miezi minne.sasa watanzania wengi huwa
wanapoteza zaidi ya miezi 9 kila mwaka ndani ya miaka 15 tayari
ameshasogeza mbele mafanikio yao kwa zaidi ya miaka kumi.kwa hiyo
ukichukuwa miaka kumi ya kutafuta maisha na ile miaka kumi aliopoteza ni
miaka 20.ameanzakutafuta maisha na miaka 30-40 miaka ya kufikia
mafanikio yake itakua 50 na maisha now ni mafupi hayafiki huko na
kipindi anaendelea kutafuta anapoteza tena masaa kadhaa.lazima ufe
masikini.amka sasa mtanzania acha kutumia muda wako vibaya kwani muda
wako unaoupoteza sasa utakugharimu.
MUDA NI MALI UKIPUUZA HILO UTAKUFA MASIKINI.ACHA KULALAMIKA CHUKUA HATUA.
Karibu tutimize ndoto zetu pamoja.
Swali msaada ushauri tumia 0715448643 au pia wawezanifuata watsap.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment