ads slot

Latest Posts:

JE UNAIJUA ELIMU ITAKAYOKUFANYA KUWA MILIONEA? SIO HADI UWE NA CHETI.

 Hatuwezi kuubadilisha ulimwengu kama hatutakuwa na elimu,hatuwezi kutimiza ndoto zetu kama hatutakuwa na elimu,watu wengi sana wanashindwa kufikia ndoto zao kwasababu ya kukosa elimu.Lakini ni kweli kuwa elimu ya darasani pekee ndio inaweza kukufanya uwe tajiri au uzifikie ndoto zako? Hapana,Wapo vijana wengi ambao wameshakata tamaa ya kufanikiwa katika maisha kwa kusingizia kuwa hawana elimu ya darasani lakini sio kweli kwamba elimu ya darasani ndio inaweza kukufanya uwe tajiri na ubadilishe maisha yako.Na wapo vijana wengi wamemaliza vyuo wamekaa nyumbani wakitegemea elimu zao tu,na wapo
wafanyakazi wamekaa maofisin wameridhika kabisa wakiamini kuwa wameshasoma wameshapata kazi inatosha bila kusahau wanajiandaa kuwa masikini watarajiwa.Kaa karibu na mimi ewe Mtanzania mwenzangu ujifunze ili ujue kama bado hujachelewa kutokwenda darasani  au kuwa na elimu hiyo moja.Amka rafiki maisha yamebadilika.USIOGOPE
Duniani kuna aina kuu tatu za elimu ambazo kila binaadam anaweza kuzitumia hizo na kuyafanya maisha yake kuwa rahisi.Elimu hizi.

  1. SCHOLASTIC EDUCATION (ELIMU YA UTAMBUZI)                                                                                      
Hii ni elimu ya darasa la kwanza hadi kidato cha sita,hii ni elimu ya darasani,ambapo ndani ya elimu hii kuna makundi mengi sana hapa wapo walioishia darasa la saba,wapo walioishia kidato cha nne,wapo waliofanikiwa kufika hadi kidato cha sita lakini wote hawa wako kwenye kundi moja tu la SCHOLASTIC EDUCATION,Kundi hili huwa tunaandaliwa kwaajili ya kujua kusoma,kuandika na kujiandaa kwenda vyuoni basi.

       2.  PROFESSIONAL EDUCATION (ELIMU YA UJUZI FLANI)
Elimu hii ni elimu ya kusomea fani fulani,mfano ualimu,udactar,uinjinia,fundi magari na zinginezo,watu wengi huamini akipata ujuzi basi maisha yake yatakuwa mazuri,lkn sio kweli kwasababu elimu hii unafundishwa ili uende kuitumikia pesa,uwe mtumwa wa kazi,na uendelee kuwafanya wengine watajirike,hautaweza kuwa tajiri kama unafikiria kuwa mfanyakazi maisha yako yote.na kama umepanga maisha yako yote kuwa muajiriwa basi umepanga kufa ukiwa masikini.kwasababu hakuna mshahara unaoweza kukufanya uzifikie ndoto zako.utaishia kwenye mikopo tu.ukisikia unataka kufukuzwa kazi unapata presha.

        3. FINANCIAL EDUCATION(ELIMU YA FEDHA)
Hahahaaaa huwa nafurahi sana kila nikiiona hii elimu kundi hili la elimu ni kundi ambalo linawatu wachache sana wenye maamuzi sahihi ya kubadilisha maisha yao.kwasababu elimu hii ndio inaweza kukufanya uwe milionea hata kama hujaenda shule,hapa utawakuta wajasiriamali na wawekezaji.Elimu hii pekee ndio mkombozi wa kila mtu mwenye hasira ya kubadilisha maisha yake,rafiki usikalie kulalamika kisa hunaelimu elimu au kazi hakuna,hii ipo na haitolewi darasani.unajifunza kutoka kwenye semina mbalimbali,na kwa watu walioendelea,watanzania wengi wanakufa masikini hata hao wanaojiona wamesoma kwasababu wamekosa elimu hii.Elimu hiii unafundishwa kuifanya pesa ikutumikie, hautaweza kuwa masikini kama pesa inakutumikia.Kama hauna elimu hii utaishia kufanya kazi kwa matajiri na kuendelea kuwatajirisha.Amka rafiki jifunze kuifanya pesa ikutumikie maisha yako yatabadilika.Utajisikiaje ukiwa wewe ndo bosi.Na inawezekana,amua sasa kubadilisha maisha yako kwa kujifunza elimu ya kuifanya pesa ikutumikie.
Inaweza kuwa unapenda kuwa na biashara yako au kujifunza elimu hii na kuwa bosi wewe au kujiajiri lkn hujui wapi uanzie au wapi upate elimu hii usijali mimi niko kwaajili ya watanzania wenzangu uwe muajiriwa au sio muajiriwa,mwanafunzi au mama wa nyumbani na unandoto za kubadilisha maisha yako.Tumia namba zangu za sim.takusaidia kupata elimu hii bila hata gharama na takufahamisha nini unapaswa kukifanya..
BADILIKA MTANZANIA AJIRA PEKEE HAITAKUFANYA UFIKIE NDOTO ZAKO
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment